Unaweza kutazama kupitia programu Mpya ya Showmax kwenye kifaa chochote cha Android hapa chini.
Muhimu: Aina ya vifaa unavyoweza kutumia kutazama Showmax inaweza kubadilika kulingana na mpango wako wa Showmax. Ili upate maelezo zaidi, angalia Kuna tofauti gani kati ya mipango ya Vifaa Vyote na Vifaa vya Mkononi Pekee?
Rununu na kompyuta kibao
- Vifaa vya mkononi vya Android vinavyotumia Android 7 au matoleo mapya zaidi.
- Huawei pamoja na HMS / Matunzio ya Programu
TV na vifaa vya kutiririsha maudhui
- Vifaa vya Android TV vinavyotumia Android 5.1 au matoleo mapya zaidi, vikiwemo:
- Smart TV zinazotumia Android TV, kama vile Sony Bravia
- Dekoda, ikiwemo NVIDIA Shield
- Vifaa vya kutiririsha mfumo wa Android TV
Muhimu: Showmax inapendekeza uangalie kwa makini kabla ya kununua kifaa chochote cha Android, kwa kuwa baadhi ya miundo inaweza kutumia mfumo wa uendeshaji ambao hautumii programu ya Showmax. Iwapo huna uhakika, angalia ikiwa kifaa kinatumia Android 4.4.0 au matoleo mapya zaidi, hakikisha kuwa kifaa hakina mizizi na uhakikishe kuwa kifaa kinaafikia Mahitaji ya Showmax ya HDCP na DRM.
Je, unatatizika kutumia Showmax kwenye kifaa chako cha Android?
Ikiwa unatatizika kuanza kutumia Showmax kwenye kifaa chako cha Android, angalia maagizo haya na miongozo ya utatuzi:
- Je, ninaweza kufanya nini kusakinisha programu ya Showmax kwenye kifaa cha Android?
- Kutatua matatizo ya kuingia kwenye akaunti
- Programu yangu ya Showmax haifanyi kazi
- Je, ninaweza kufikia Showmax katika nchi gani?
Muhimu: Kwa sasa huwezi kujisajili kwenye Showmax kwenye programu ya Showmax. Angalia Nitafuata hatua gani kujisajili kwenye Showmax ili upate hatua za jinsi ya kujisajili kupitia tovuti ya Showmax, kisha utumie maelezo ya akaunti yako mpya kuingia kwenye akaunti kwenye kifaa chako cha Android