Sasa unaweza kujiandikisha kwenye Showmax ukitumia Vodacom:
- Bonyeza USSD ya Vodacom kwenye *149*01*33#.
- Chagua Mpango wa Showmax unaokufaa.
- Chagua usajili wa kila mwezi au kila wiki.
- Chagua chaguo la malipo: M-Pesa au Lipa ukitumia Muda wa Maongezi.
- Ikiwa umechagua M-Pesa, weka PIN yako ya M-Pesa. Ikiwa umechagua Lipa ukitumia Muda wa Maongezi, hutahitaji PIN.
- Bofya kiungo kilichotumwa kupitia SMS ili ikupeleke kwenye tovuti ya Showmax. Ikiwa tayari una Akaunti ya Showmax ingia tu, au ikiwa wewe ni mteja mpya basi fuata hatua ili ufungue Akaunti yako ya Showmax.
- Usajili wako unaendelea, na uko tayari kuanza kutazama.
Muhimu: Iwapo una njia inayotumika ya kulipa, utahitaji kwanza kukatisha mpango huo wa kulipishwa kabla uchague mshirika mpya wa ulipishaji.